• Call us: +255 754 618 809
  • Email: info@seditvicoba.or.tz
SEDIT Vicoba
SUPPORT US
  • Home
  • About Us
    • About Us
    • Mission and Vision
    • Services
    • Objectives
    • Our Tools
    • Organization Structure
    • Our Team
  • Programmes
  • Partners
  • Blog
    • News and Events
    • Publications
    • Videos
  • Contact Us

SEDIT VICOBA SULUHISHO LA UMASKINI

  /   News & Events   /   SEDIT VICOBA SULUHISHO LA UMASKINI
Mar 09, 2020
SEDIT VICOBA SULUHISHO LA UMASKINI
09Mar

WANANCHI Jijini Tanga, wameelezwa kwamba suluhisho pekee la kuondokana na umasikini ni kujiunga na Mpango wa Kukopeshana Sedit Vikoba ambao umeonesha watu wengi kujiendeleza kiuchumi katika familia zao.

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa vikundi vya Vikoba vilivyopo katika Jiji la Tanga uliofanyika juzi kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tanga Eckernforde, Mwenyekiti wa shirikisho la Vikoba nchini George Sweveta, alisema ili watuwaondokane na umasikini ni kujiunga kwa wingi na mpango huo.

"Ndugu zangu wana-Tanga, mmechagua mlango sahihi kwa kujiunga na mpango huu wa Vikoba, mkivitumia vizuri kwa kufuata masharti yake na taratibu zake mnaweza kuwa matajiri kama watu wengine," alisema Sweveta ambaye kabla ya mkutano huo alivitembelea vikundi takribani 30 vilivyo Jijini hapa.

Alisema kuwa ili Vikoba katika Jiji la Tanga viweze kuinuka na wananchi kuondoa umasikini wameandaa mkakati wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wana-kikundi ambao kupata kwao mafunzo hayo kutawaweka kujua mbinu na taratibui za kuendesha vikoba kisasa na kitaalamu zaidi.

"Ni vema mkaelewa mbinu za kupanda na kusimamia mambo ya uchumi...Sababu mnaweza kuweka na kupata fedha nyingi za mkopo lakini mkashindwa namna bora ya kurejesha mikopo hiyo, lazima muwe tayari kujifunza kutoka Sedit-Vikoba," alisema.

Alisema shirika la Sedit Vikoba wameliunda tangu mwaka 2002 katika wilaya ya Kisarawe na Zanzibar ambapo wadhamini wakubwa ni wanachama wenyewe, serikali na wafadhili mbalimbali watakaojitokeza kufuatia wanachama kufanya vizuri katika michango yao.

Mwenyekiti wa vikundi vya Sedit-Vikoba katika Tanga Dkt Ali Buge na katibu wake Elda Kishimbo, aliwata wana-Vikoba katika Jiji la Tangakwa kushirikiana kuhakikisha lengo la kuondokana na umasikini linafanikiwa kupitia mpanmgo huo.

Vikoba hivyo wamepanga Novemba 11 kuvizindua rasmi kwa kumwalika kiongozi mkubwa wa serikali katika sherehe ambayo wanatarajia kwamba itafana kutokana na kwamba vikundi vingi vitaongezeka.

Other Posts

  • 4 years ago Microfinance and health services: Experience and views of women in the VICOBA grassroots bank system
  • 5 years ago Vicoba Week and Trade Fair - Nov 2020
  • 6 years ago New project to improve SMEs in S.A, Zambia and TZ launched SADC
  • 7 years ago Vicoba Week and Trade Fair - 2018
  • 7 years ago SEDIT VICOBA WEEK & TRADE FAIR 2018

Categories

  • News and Events4
  • Publications1
  • Opportunities0
  • Videos1

Facebook

Social Connect

SEDIT Vicoba

Main Office

  • Ilala Bungoni, Dar es Salaam
  • info@seditvicoba.or.tz
  • +255 22 2863271
  • +255 754 618 809

Our Branches

Dodoma Zonal Office
Off - Morogoro Road (Behind St Gaspar Hotel),
Plot48 - Kisasa Street, Dodoma.
Mob: 0673-741547

Geita Field Office
Plot No. 0055 - Katoma Street,
Bomani Road - GEITA.
Mob: 0629-533350

Our Branches

Masasi Zonal Office
Southern Zone,
Masasi – Mtwara.
Mob: 0716-250216

Mwanza Zonal Office
Airport Road - Pasiansi,
Majengo Mapya llemela, Mwanza.
Mob: 0713-791622

Quick Links

  • About Us
  • Mission and Vision
  • Services
  • Objectives
  • Our Tools
  • Organization Structure
  • Our Team
  • Our Partners
  • Programmes
  • News & Events
  • Contact Us
  • Our Locations
  • Privacy Policy
Copyright © 2026 - SEDIT Vicoba